Baada ya kupoteza mechi dhidi ya Simba, klabu ya Yanga itashuka dimbani dhidi ya Ruvu shooting leo.
Mbali na maneno ya vitisho dhidi ya msemaji wa Ruvu Shooting Masau Bwire, lakini Yanga itashuka kamili uwanjani leo.
Bado Yanga haijapoteza matumaini ya kutetea ubingwa wao siku ya leo, na endapo watashinda mchezo huo wa mkononi watapunguza uzito wa pointi 3 kutoka kwa simba ambayo itakuwa kileleni kwa pointi 2 dhidi ya wababe hao.
Yanga itaikaribisha Ruvu Shooting katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo mechi hiyo itachezwa majira ya saa 10 za jioni.

Comments
Post a Comment