Azam ipo kamili kuivaa Mbao FC.


Mei 5, 2017

Kikosi cha Azam FC kipo kamili kuivaa Mbao FC katika mchezo wa ligi kuu utakaopigwa kesho katika uwanja wa Chamanzi Complex majira ya saa 1.00 za jioni.

Kocha wa timu hiyo Aristica Cioaba amesema kuwa walishasahau watokeo ya nusu fainali ya FA dhidi ya Simba na sasa wanajikita kusaka ushindi dhidi ya Mbao.

"Niliwaambia wasahau matokeo yale na sasa akili yetu ni kupata ushindi dhidi ya Mbao FC.

"Kikosi kipo kamili ingawa tunamkosa Himid Mao ambaye ameenda kwenye majaribio, kwa ujumla wachezaji wote wapo kamili kwa mchezo huo." Alisema Cioaba.

Azam itashuka uwanjani ikiwa na kumbu kumbu ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Mbao baada ya kufungwa bao 4 katika uwanja wa CCM Kirumba.

Comments