Timu ya Azam FC leo imeanza ziara yake nchini Uganda ambapo watacheza mchezo wa kirafiki na KCCA ya Uganda katika uwanja wa Philip Omondi jijini Kampala.
Azam imeweka kambi ya siku 10 nchini humo ikiwa ni sehemu ya maandilizi kuelekea ligi kuu Vodacom ambayo itaanza kutimua vumbi Agosti 26 mwaka huu.
Mbali na mechi hiyo Azam pia itacheza na Onduparaka hapo kesho, URA agosti 14 na Vipers agosti 15.

Comments
Post a Comment