Aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga Malimi Busungu amejiunga na timu ya Lipuli kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Busungu aliyewahi kuwika akiwa na Mgambo ya Tanga pamoja Young Africans alipoteza mvuto uwanjani kutokana na kukumbwa na majeraha ya mara kwa mara.
Baada ya kumaliza mkataba wake Yanga mchezaji huyo tutamuona tena ligi kuu akiiwakilisha lipuli ambayo imepanda kushiriki ligi kuu.msimu huu.

Comments
Post a Comment