Chelsea yachemka kwa Burnley, yapigwa 3-2.


Chelsea imeshindwa kutamba katika uwanja wa nyumba ukiwa ni mchezo wake wa kwanza ligi kuu baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-2.

Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Chelsea ilikuwa imepigwa mabao 3-0, ikiwemo na kadi nyekundu ambayo alipewa Gary Cahil.

Chelsea ilipata ahueni baada ya kuingia Alvaro Morata ambaye aliweza kuipatia Chelsea bao la kwanza la kusawazisha katika dakika ya 69 na baadae David Luiz katika dakika ya 88.

Ushindi huo umekuwa wa kwanza kwa Burnley ambayo haijawahi kuifunga Chelsea ikiwa nyumbani tangu mwaka 1998.

Comments