Manchester City ni kama imeanza kupokea cha changamoto za ligi kuu England baada ya kulazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya Everton.
Wayne Rooney ambaye amenza kuwa moto aliipatia Everton bao la kuongoza katika dakika ya 35 kipindi cha kwanza.
Manchester city iliingia kwenye kipindi kigumu kwa mara nyingine baada Kyle Walker kulimwa kadi myekundu katika dakika ya 54.
Hata hivyo Manchester city ilipambana na kupata bao la kusawazisha kupitia Raheem Sterling aliyefunga katika dakika ya 82.
Siku tatu kabla ya mchezo huo kocha wa Everton Ronald Koeman alitamba kuwazuia Manchester city kutokana na kuzisoma vema mbinu za Pep Gurdiola.

Comments
Post a Comment