Mwaka huu unaweza kuwa wa shetani kwa mshambuliaji Diego Costa ambaye ametolewa nje katika usajili wa Atletico Madrid chini ya kocha wao Diego Simeone.
Simeone amekana kuwepo kwa mpango wa kumrejesha strika huyo Vicente De Calderon baada ya kuachwa na kocha wa Chelsea.
Diego Costa mwenye miaka 27 aliweka matumaini makubwa ya kuungana na kocha wake huyo wa zamani ambaye kwa mujibu wa vyanzo vya habari amesema kuwa hana mpango wa kumrejesha Costa Calderon.
Mapema baada ya kumalizika kwa ligi Diego Costa aliweka wazi nia ya kocha Antonio Conte ambaye alimtumia ujumbe kuwa hatakuwepo kwenye mipango yake msimu huu.

Comments
Post a Comment