Cannavaro: Uwanja umetunyima matokeo mazuri zaidi


Nahodha na beki kisiki wa Yanga Nadir Haroub 'Cannavaro' amesema kuwa uwanja ndiyo uliyowanyima matokeo mazuri zaidi dhidi ya Kagera Sugar hapo jana licha ya kupata ushindi wa bao 2-1.

Mchezo huo uliambatana na mvua kubwa ambayo ilisababisha uwanja wa taifa kujaa maji na kupoteza uelekeo wa mpira mara kadhaa ikiwemo na wachezaji kuteleza.

Nadir alisema kuwa sababu ya kupoteza nafasi nyingi walizotengeneza ni kutokana na uwanja wa kujaa maji na hivyo wachezaji walipoteza pasipo matarajio halisi.

"Tumepata nafasi nyingi lakini hali ya uwanja haikuwa nzuri, uwanja umejaa maji kutokana na mvua na hii imetufanya kupoteza nafasi nyingi.

"Pamona na yote tumefanikiwa kutoka na pointi tatu na hilo ndilo jambo muhimu, tumerejea kileleni dhidi ya mpinzani wetu simba." Alisema Nadir

Comments