Kama una jambo lako na umelala nalo kitandani, Bwana atakuacha hapo ulemewe na usingizi. Kufanikiwa na kuinuka utasikia kwa wengine.
Hata ukikesha kumwomba Bwana usiku na mchana, bila hatua zako Bwana hatoanza kukanyaga, atakusubiri ukanyage kwanza, ndipo ataongeza kishindo cha hatua zako na Yeye atakanyaga zaidi mbele yako.
Unapomwamini, Bwana wala hataki maswali yako kama utaweza au utashindwa. Yeye ana jibu moja tu, anaweza, siku zote ni mshindi.
Huwapa ushindi wale Askari hodari, huwapa ushindi walio tayari, Mungu husimama na hata mtu mmoja katika jeshi kamili ikiwa yupo tayari kuchukua hatua. Wenye kufanya maamuzi ndiyo ambao Bwana huanza nao kwenye safari yao mafanikio.
Wakoma wanne wanafanya hawajali watakufa ama wataishi wanainua hatua zao, na ndipo Bwana anakanyaga kwa kishindo juu yao. Tazama maandiko 👇🏾
2 Wafalme 7:6
" _Kwa maana Bwana alikuwa amewasikizisha Washami kishindo cha miendo ya magari, na kishindo cha farasi, kama kishindo cha jeshi kubwa; wakaambiana, Tazama, mfalme wa Israeli amewaajiri wafalme wa Wahiti, na wafalme wa Wamisri, waje wapigane nasi."
Kama una biashara yako, maono yako, ndoto zako, mipango, na umwamini Bwana fanya maamuzi sahihi. Mafanikio hayaji kwa kujaribu ukiwa umelala kitandani. Amua leo
> Kuinua hatua zako
> Amini wewe unaweza
> Achana na maswali ya kushindwa
> Usipuuze mawazo yako ya biashara bila kuyajaribu
> Usiogope anza kujiamini
> Amina kwamba Mungu yupo pamoja na wewe
> Itazame ahadi Bwana kwako kuwa timilifu
Bwana anahitaji watu imara katika maamuzi, walio tayari kuinua hatua zao. Bwana hukanyaga pamoja nao wale walio tayari, kwa moto wa kishindo cha wakoma na ushindi
Imeandaliwa;
Ev: Emanuel Saulo
0718143834
Makabe, DSM

Comments
Post a Comment