Coastal union yaichakaza yanga, Simba yang'ara taifa


Timu ya Coastal union leo ikiwa katika uwanja wake nyumbani mkwakwani mkoani Tanga iliibuka kifua mbele bada ya kuichapa timu ya Yanga kipigo cha mabao 2-0.

Mabao hayo yaliwekwa nyavuni na Miraji Adam katika dakika ya 27 na lile la pili lilitumbukizwa nyavuni na Juma ambaye alifunga kwa kupiga shuti kali lililomshinda kipa wa Yanga Deogratius Munishi na kuingia wavuni na hivyo kukamilisha ushindi wa mabo 2-0 kwa Coastal union.

Wakati Yanga ikipoteza mchezo watani wao jadi simba wakiwa katika uwaja wa taifa waliweza kuichaza African sports ya Tanga baada ya kuichapa kipigo cha mabao 4-0. Mabao ya Simba yalifungwa na Hamis Kiiza aliyefunga goli 2, Hassan Kessy na Haji Ugado ambaye alikamilisha ushindi huo wa magoli 4 katika dakika ya 75 ya mchezo.

Matokeo hayo yanaiwezesha Simba kumnyatia nyuma mpinzani wake Yanga kwa pointi 3. Yanga ipo juu kwa pointi 39 ikilingana na Azam huku Simba ikiwa imesogea hadi pointi 36 nyumba ya miamba hao.

Comments