Gurdiola atatua man united au city?



Kocha wa Bayern Munich Pep Gurdiola alikataa kusaini mkataba mwingine na mabingwa hao wa Ujermani, nia yake ikiwa wazi kabisa anataka kuondoka katika timu hiyo nakufundisha klabu uku matazamio ya wengi ni hamu ya kumuona kocha uyo aliyewika na barcelona akielekea katika ligi ya Uingereza.

Mancity wameonesha nia kubwa ya kumchukua kocha huyo ambaye amekuwa akifanya vizuri kila anakopita, mancity inaamini kocha Pep atakata kiu yao ya kuwania taji la mabingwa barani Ulaya, ambapo tangu ijihakikishie kupata nne bora imeshindwa kufanya vizuri kwenye michuano hiyo.

Wakati huu ambao kocha wa man united Luis vaan gaal anashindwa kufanya vizuri chini ya kocha huyo bila shaka kiu yao ni kutaka kumwona kocha huyo fundi analeta mbinu zake old trafford ili kurejesha heshima yao waliyoipoteza kwa misimu 3 sasa.

Si man united pekee bali hata tajiri wa chelsea Roman Abromovich anafikiria kumlete kocha huyo kwa miamba hiyo ya darajani ili alete soka safi ambalo anatamani kuliona likichezwa pale darajani na ana mpango kama ule wa city wa kumfanya Pep awe analipwa zaid kuliko makocha wote duniani

Hofu yangu ni kuwa Gurdiola hapendi presha nina uhakika anaweza kutua Etihad badala ya Stamford bridge au Old trafford, licha ya mafanikio aliyonayo city lakini haina presha kulinganishwa na ile ya Man united na chelsea.

Mancity haina presha licha ya kocha Pellegrin kutofanya vizuri msimu huu ana amani katika kazi yake tofauti na wakati ule mgumu alioupitia kocha Jose Mourinho kabla hajaondoka chelsea na hii presha anayoipata LVG wakati huu.

Mancity ni timu kubwa lakin haizid manchester united na Chelsea hata kwa namba za mashabiki dunian ni wazi united na chelsea ziko juu kuliko city, nadhani anachofikiria Pep atakuwa na wakati mzuri akiwa na city kuliko united na chelsea.

Ikumbukwe Ferguson ndiye mfalme wa old trafford, nadhan Gurdiola anataman ufalme wake pale city kuliko kukaa united ba kulifunika ilo jina kubwa lililokaa vichwan mwa mashabiki wa united na linaweza kukaa milele.

Comments