Mashabiki wa timu ya Stand united walileta vurugu na
kupelekea kusimama kwa mchezo wa kombe la FA uliochezwa jana dhidi ya mwadui fc
katika uwanja wa Kambarage mkoani shinyanga.
Vurugu hizo zilitokea dakika ya 88 ya mchezo baada
ya mashabiki hao kutoridhishwa na maamuzi ya mwamuzi wa mchezo huo ambaye
alionekana kuipendelea timu ya Mwadui fc baada ya kutoa penati katika dakika ya
65 na kukataa bao la kusawazisha kwa Stand united dakika 88 kutokana na Elias Maguli
kuunawa mpira kabla ya kutoa pasi ya goli na kupelekea mchezo huo kusimama kwa
takribani dakika saba.
Kocha wa stand stand united Patrick Liewing alijihami kwa kukinga kichwa chake na kiti
kutokana na kurushwa kwa mawe na chupa za maji uwanjani kutoka kwa mashabiki
waliokuwa wamejawa na hasira baada ya kutoridhishwa na mwenendo wa mchezo.
Mchezo huo uliendelea baada ya jeshi la polisi
kuimarisha ulinzi na usalama na kurejea kwa amani ya mchezo, hadi mwisho wa
mtanange huo Stand united ilishindwa kusawazisha bao pekee lililowekwa nyavuni
kwa mkwaju wa penati na Jeryson Tegete na hivyo kuyaaga rasmi mshindano
hayo.

Comments
Post a Comment