Kiungo wa klabu ya chelsea Ramires ameiaga timu yake rasmi baada ya kujiunga na timu ya Jiung Siung ya nchini china kwa dau la paundi 22.5 milioni baada ya miaka 6 akiwa na uzi wa bluu.
Ramires alijiunga na chelsea akitokea Benifica ya ureno Agosti 2010 kwa dau la paundi 19 wakati chelsea ikiwa chini ya kocha Carlo ancelloti.
Ramires amefikia uamuzi huo baada ya kukosa namba ya kudumu kikosin chini ya kocha mpya Guus Hiddink ambaye alimtumia katika mechi waliyotoa sare dhidi ya Manchester united.
Kuondoka kwa Ramires Chelsea kunaongeza uhakika wa maisha zaidi kwa kiungo Obi Mikel ambaye alikuwa na wakati mgumu chini ya kocha Jose Mourinho

Comments
Post a Comment