Usajili wa maji ya jioni, kabla ya kufungwa kwa dirisha

Leo majira ya saa 5 usiku dirisha la usajili litafungwa rasmi lakini bado zipo heka heka za usajili wa baadhi ya wachezaji ambao huenda mipango ya usajili inaweza kukamilika muda wowote kabla ya kufungwa kwa dirisha hilo

Jack Wilshere 

Baada ya kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Arsenal kutokana na ujio wa Granit Xhaka aliyesajiliwa kwa dau la paundi 30 milioni, nyota huyo wa Englang amepewa nafasi  na kocha Arsene Wenger kuchagua timu yoyote atayopenda kucheza kwa mkopo wa mwaka mmoja ili kurejesha kiwango chake. Crystal Palaca na AFC Bournemouth ndiyo zinaongoza kwenye mbio kumwania Wilshere 24, kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili huenda tukapata jibu.

Moussa Sissoko

Nyota huyu mwenye miaka 27 ambaye ni raia wa Ufaransa haoneshi kuridhishwa kubaki na
Newcastle ambayo kwa sasa inashiriki ligi daraja la kwanza. kiwango bora alichokionesha mfaransa huyo kwenye michuano ya UEFA Euro kuna rejesha imani kwa Sissoko ambaye anaamini thamani yake ni kucheza ligi kuu. Tottenham ndiyo inayoongoza kwenye mbio za kumwania mchezaji huenda tukasikia lolote kabla ya kufika saa 6 za usiku.

Wilfrey Bony

Raia huyu wa Ivory Coast ameshindwa kutamba kwenye timu mpya ya Gurdiola, ni wazi mshambuliaji huyo hana nafasi mbele ya Sergio Aguero pamoja na Kelechi Ihenacho ambaye anachipukia kwa kasi. Kwa sasa mchezaji huyo yupo kwenye mazungumzo na timu ya Stoke city huenda tukasikia lolote kabla ya kufungwa kwa dirisha hilo.

Wachezaji waliokamilisha uhamisho hadi sasa

Joe Hart ametua kwa mkop katika timu ya Torino inashiriki ligi ya Serie A nchini Italy

Gokan Inler ametua Besiktas akitokea Leicester

Comments