Simba sports inaweza kuwa bingwa?

Wapenzi wa klabu ya simba bado wana kiu kubwa ya kupata ubingwa msimu huu, lakini hawana imani kama klabu hiyo inaweza kuchukua ubingwa na kurejesha heshima yake katika ule mtaa wa msimbazi. mpaka sasa simba imekusanya idadi ya pointi 30 katika michezo 15 iliyocheza raundi ya kwanza ikiwa chini ya Azam na Yanga kwa pointi 6.

Kwa mtazamo wa soka huku zikiwa zimebaki mechi 15 za raundi ya pili huwezi kuitoa klabu ya simba kwenye mbio za ubingwa  kwa kuwa imeachwa kwa pointi 6 ikiwa  ni idadi ya mechi 2 pekee,  kama Yanga au Azam itapoteza na timu hiyo ikashinda  michezo hiyo bila shaka wanaweza kuwa pamoja kwenye mbio hizo.

Ni mambo gani yanayoikwamisha simba kwenye mbio za ubingwa?

Safu ya ulinzi

Bado kuna tatizo katika safu ya ulinzi kwenye klabu ya simba, licha ya Mohamed Hussein (Tshabalala) na Emery Nimuboma kufanya vizuri upande wa kushoto na kulia lakini bado kuna makosa katika beki ya kati. Juko Murshed anahitaji kupata beki anayepambana kama ilivyo kwa KevinYondani kutoka yanga au Pascal Wawa kutoka azam bado Hassan Isihaka ana mapungufu mengi hususani mwili na kimo chake kinamfanya ashindwe kumudu mipira ya juu na amekuwa na mahesubu finyu katika kuziba nafasi za wapinzani ikumbukwe makosa yake yaliigharimu simba katika mechi yake dhidi ya Azam na Toto Afrika pale mwanza na huo ndio ulikuwa mwanzo mwanzo wa kocha Kerry kumweka benchi na kumtumia Abdi Banda.

Hawajitoi na kupambana

Wachezaji wa simba wamekuwa ni wenye kukata tamaa mapema na hiyo imekuwa ikiwagharimu mara kadhaa, Claudio Ranieri amewahamasisha wachezaji wa Leicester city kupambana, ikumbukwe hawana nyota anayelipwa kiwango cha Ronaldo wala Rooney lakini wakati wote wamejitoa na kuipigania timu yao juhudi zao ndizo zinazowaweka pale juu ya msimamo wa EPL, hivi ndivyo simba inavyotakiwa kuwa ipambane na kujitoa ili kupiku Azam na Yanga katika mbio za ubingwa.

Hawana kasi ya kushambulia

Mfano mzuri ni timu ya Azam haichezi mpira mzuri katikati kama ule wa simba lakini wanashambulia kwa kwa nguvu na hii inawafanya kupata matokeo bora wakati wote, kama kocha wa simba hataongeza mbinu zaidi katika kushambulia basi ni wazi itadondoka kwa kuzoa sare nyingi ambazo hazitawapa ubingwa, wazungu wanasema "force 9" naiona kwa Yanga na ndio maana wanapata matokeo mazuri wakati wote katika mechi zao. Jackson Mayanja anahitajika kumtumia vizuri Hamisi kiiza kupitia Ibrahimu Ajibu na Danny Lyanga.

Hawana mchnganyiko

Wazungu wanaitwa"chemistry" huu ni mchanganyiko ambao hujengwa kutokana na kuwa na first eleven iliyoshiba yaan kikosi cha ushindi, kama ilivyokuwa ile Andy Cole na Dwight Yorke pale Man united au ile  ya Steven Gerrard na Fernando Torres wakati ule wa Rafaeli Benitez akiwa na Liverpool yaan ni kujua kujua namna gani ya kucheza na kushamulia kutokana kucheza pamoja mud mrefu hii ndio tatizo lingine ambalo linaukumba simba, mfano pale Yanga ni rahis kwa Donald Ngoma, Amis Tambwe na Simon Msuva kutengeneza magoli kuliko pale simba kwa sababu wanacheza pamoja muda mrefu.


Kama simba watayafanyia kazi mambo haya machache inawezekana wakawania ubingwa msimu huu, wanatakiwa kupambana kuhahakisha wanapata matokeo muda wote naikumbuka ile kauli ya nahodha wa Yanga Nadir Ayoub alisema "ni bora kucheza vibaya lakini upate matokeo kwa kuwa pointi 3 ni muhimu zaidi" alizungumza hayo baada ya ushindi dhidi ya Coastal union baada ya kushinda bao moja ambalo liliendeleza ndoto za ubingwa wao msimu wa 2014/15.

Comments