Timu ya Chelsea imeanza kufanya mazungumzo na kocha wa timu ya taifa ya Italy Antonio Conte kumshawishi kocha huyo atue London ili awanoe wababe hao wa darajani.
Kuna uvumi kuwa Chelsea imesafiri rasmi ili kuuvunja mkataba alionao kocha dhidi ya timu ya taifa ya Italy ili kumpatia ofa mpya ya kuwanoa wababe hao wa London ambao wako chini ya kocha muda Guus Hiddink.
Conte 46, amewahi kuinoa Juventus ambayo ilirudi kwenye chati baada ya kupoteza heshima yao kwa misimu kadhaa, kabla ya kuiacha timu hiyo kwa Massimiliano Allegri, Conte alikuwa amebeba mataji matatu mfululizo ya Serie A.

Comments
Post a Comment