Coastal yaipaisha simba kileleni


Timu ya Simba imeendelea kubaki kileleni katika msimamo wa ligi kuu ya Vodacom baada ya timu ya Azam kukubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Coastal union katika mchezo uliochezwa jana katika uwanja wa mkwakwani mkoani Tanga.

Azam ilifungwa bao hilo katika dakika ya 68 na Miraji Adam baada ya makosa yaliyofanywa golikipa wao Aishi Manula. Matokeo hayo yanaifanya samba kubaki juu ya msimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi 45 ikifuatiwa na Yanga yenye pointi 43 ambayo ina mchezo mkononi.

Hata hivyo timu ya Azam bado ina akiba ya michezo 2 mkononi ambayo ilishindwa kucheza baada ya kualikwa kwenye michuano iliyofanyika nchini Zambia na kama itashinda michezo iliyowekwa kipolo bado itakuwa na nafasi ya kuwa juu ya msimamo na kuziacha timu za Simba na Yanga.

Mechi za ligi kuu znatarajiwa kuendelea tarehe 20 ya mwezi huu ambapo kutakuwa na mchezo mkali utakao wakutanisha mahasimu na watani wa jadi wa Tanzania Simba na Yanga.

Comments