Europa ligi kuitunisha misuli Liverpool, Man united.


Liverpool na man united zimejikuta zikikutana tena katika michuano ya Europa ligi baada ya timu zote kufuzu katika raundi ya 32 na hivyo mtanange huo kujirudia kwa mara nyingine katika hatua ya 16 bora  baada ya kumaliza mechi za EPL.

Ikiwa ni misimu miwili sasa tangu kutua kwa kocha Luis van Gaal pale Old Trafford Liverpool haijawahi kupata ushindi dhidi ya LvG. Mechi inaweza gumzo na kitendawili kuwa nani ataingia hatua ya robo fainali baada ya kumshinda mwenzake.

Inawezekana wapenzi na mashabiki wa Man united wana matumaini zaidi kuliko Liverpool licha ya mashetani kushindwa kuwa na timu ya kuridhisha lakini imepata matokeo bora dhidi ya Liverpool ikiwa ni misimu miwili sasa dhidi ya Liverpool.

Baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya Liverpool kocha wa Man united LvG alinukuliwa akisema hana presha na Liverpool kwa kuwa ni timu inayompa matokeo wakati wote. Nakumbuka mtanange wao katika mechi ya marudiano pale Anfield licha ya Liverpool kufungwa goli 1 pale anfield lakini iliweza kucheza mpira mwingi ulikuwa ni uzembe wa Liverpool kushindwa kuzitumia nafasi za kufunga ipasavyo.

Liverpool ikiwa chini ya kocha Jurgen Klopp ina soka la pasi za haraka na kasi ikiwa hailingani na ile iliyoachwa na Brendan Rodgers, ni wakati huu ambao kuna kitendawaili kidogo kuhusu mtanange huo utakaporudiwa kwa mara nyingine.

Tangu kutangazwa rasmi kwa mshindi wa kombe la kombe la Europa imetoa rasmi nafasi kwa bingwa wa michuano hiyo kupata nafasi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa barani Ulaya hali pekee inayoleta ushindani mkali katika michuano ilitoa nafasi kwa Sevilla alipobeba ubingwa huo dhidi Dnipro.

Klopp alitangaza rasmi ikiwa ni wiki moja imepita kuwa kushinda taji hilo ndiyo nafasi pekee  aliyonayo ili kuipeleka Liverpool katika michuano ya klabu bingwa Ulaya, hivyo anaipanga Liverpool kupigania nafasi hiyo waweze kurejea katika ligi ya mabingwa baada ya kuwepo kwa uwezekano mdogo kuingia nne bora katika ligi ya EPL.

Jambo hilo si kwa Liverpool pekee hata Man united inahitaji kushinda taji hilo ili ijihakikishie kushiriki michuano ya mabingwa barani Ulaya, mpaka sasa Man united inasuasua katika safari yake ya kuingia nne bora ili kushiriki michuano licha ya kuwa katika sehem nzuri ya msimamo wa ligi ya EPL kuliko Liverpool lakini bado timu hizo hazina uelekeo rasmi kuwa huenda zikaingia nne bora.

Licha ya ushindani , kutafuta heshima na upinzani walionao lakini taji la Europa linawahusu kuondoa matatizo yao ambayo yanawakumba au yanaweza kuwakumba na ndiyo maana nina uhakika mtanange huu utakuwa mkali zaidi ya ule wa EPL kwa kuna fursa yenye kutafutwa na timu zote mbili ambazo zimekuwa na uelekeo mbovu katika ligi ya EPL.

Comments