Hii Azam ni kama city ya Mancin


Watu wanashangazwa na timu Azam licha ya kutofungwa hadi sasa tangu kuanza kwa msimu wa ligi kuu wa 2015/16 lakini ni timu isiyocheza mpira wa kuvutia uwanjani ikiamini zaidi katika matokeo, kuliko kucheza mpira mwingi katikati kama ilivyo katika timu ya Simba, Yanga na Mtibwa.

Kocha Stewart Hall amekuwa akilinda zaidi na kushambuliaji kwa count attack hii imeifanya Azam kuwa timu ngumu kupoteza matokeo, ulinzi imara wa Pascal Wawa, safu ya kiungo ya Iddy Mao, Mudathir Yahya na Jean-Baptiste Mugiraneza unanikumbusha mifumo migumu ya Roberto Mancini alipokuwa na mnchester city.

Mancini alikaba zaidi na kushambulia zaidi idadi ndogo ya magoli ya kufungwa na ile kubwa ya magoli ya kushinda ndiyo iliyomwinua Mancini na kunyanyua ubingwa wa ligi kuu Uingereza na kumpiga chini Ferguson ambaye alilingana pointi na timu ya Mancini na kuzidiwa idadi ya magoli.

Licha ya kuibuka na ushindi wa idadi ndogo ya magoli lakini si wepesi wa kupoteza mechi zao na wamekuwa wakipata matokeo katika viwanja vya mikoani na nyumbani, hii ni kutokana na ulinzi imara wa timu hiyo. Mancini alitumia viungo wengi na wa kazi pale katikati akiwemo Gareth Barry, Raul Garcia, Yaya Toure na David Silva.

Sterwart anawatumia viungo wengi pia na hivyo Azam imekuwa ngumu kupitika hasa eneo lao la ulinzi na eneo lake la ushambuliaji lipo imara likiwa chini ya Faridi Mussa, Kipre Tchetche na John Bocco. kama Azam itapata matokeo hayo mpaka mwisho wa msimu na kuibuka bingwa bila shaka kocha Roberto Mancini atakuwa ametembea na Sterwart Hall na hii ndiyo Azam inayofanana na Manchester City iliyotwaa ubingwa mwaka 2012.

Comments