Gianni Infantino ndiye Raisi mpya wa FIFA baada ya kuibuka kidedea jana dhidi ya mpinzani wake namba mbili Sheikh Salman bin Ibrahim al-Khalifa, huyu ndiye mteule mpya ambaye anaziba rasmi nafasi hiyo iliyokuwa chini ya Sepp Blatter.
Gianni Infantino 45, mwenye asili ya Kiswiss na Kiitaliano amewahi kuwa katibu mkuu wa chama cha soka barani Ulaya (Uefa) tangu mwaka 2009 na amekuwa mwongozaji wa sherehe za kuchezesha draw za timu mbalimbali katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.
Infantino ameweka wazi mpango wake kuongeza idadi ya timu zitakazoshiriki kombe la dunia kutoka idadi ya timu 32 hadi 40 na kujaribu kuweka usawa katika vyama vya soka duniani
"siwezi kueleza ninavyojisikia baada ya kuchaguliwa kuibeba dhamana hii" aliiambia FIFA
"Dunia itashangazwa kwa jinsi tutakavyoingoza fifa na hakika tutasifiwa kwa kazi nzuri tutakayoifanya, nimepitia mengi ambayo sikutarajia na kukutana na watu wengi wa kushangaza ambao pumzi na maisha yao ni soka na wengi wanastahili kuiona FIFA ikiwa juu wakati wote" aliongeza Infantino
Rais huyu mpya wa FIFA alichukua rasmi nafasi ya Michael Platini baada ya kufungiwa kutojihusisha na msuala ya soka kwa muda wa miaka 6, lakini ni rafiki wa karibu sana wa Michael Platin ambaye amefungiwa kujihusha na masuala ya soka.
Gian Infantino anakuwa Mswiss mwingine ambaye anakalia cheo hicho baada ya Sepp Blatter ambaye ndiye aliyekuwa akishikiria nafasi hiyo. Giann Infantino ni mkazi wa huko Valais region nchini Uswiss ikiwa ni umbali wa mile 6 kutoka mahali anapoishi aliyekuwa raisi wa FIFA Sepp Blatter.
Licha ya kufungiwa kwa aliyekuwa raisi wa soka barani Ulaya Michael Platini, Rais mpya wa FIFA Giann Infantino ameweka wazi amefanya kazi na Platini kwa miaka 9 na kusisitiza kuwa Platini alikuwa mchapa kazi na amejifunza kujiamini kupitia Platini ambaye amefungiwa kujihusisha na masuala ya soka kwa sasa.

Comments
Post a Comment