Liverpool inakaribia kukamilisha usajili wa mchezaji Joel Matip anayekipiga katika timu ya Shackle 04 katika ligi ya Bundesliga nchini Ujermani,
Matip 24 ni mzaliwa wa Ujermani mwenye asili ya Cameroon ambaye anaweza kucheza kama beki wa kati na kiungo mkabaji na amekuwa kwenye wakati katika kikosi cha Schackle 04 hali iliyopelekea timu ya Liverpool kumuhitaji katika timu yao.
Usajili huo umekuja baada ya Liverpool kuwa na safu duni ya Ulinzi na hivyo wameamua kumsajili nyota wakiamini atashirikiana vema na Martin Skrtel kuimarisha na kuunda safu bora ya ulinzi kwa vijogoo hao wa Merseyside.
Mbali na usajili wa mchezaji huyo bado kocha Jurgen Klopp ana mipango ya kuongeza mshambuliaji mwenye kasi baada kushindwa kuwika kwa mshambuliaji Christian Benteke na Jamie Vardy pamoja na Mauro Icardi wamekuwa katika mipango yake.

Comments
Post a Comment