Kocha wa timu ya Liverpool Jurgen Klopp amesema kuwa hajarishwa na kiwango kilichooneshwa na timu yake jana ilipokuwa ikimenyana na timu ya FC Augsburg ya Ujermani baada ya kushindwa kupata goli na matokeo kuwa sare.
akizungumza mara baada ya mechi Klopp amesema kuwa Liverpool ilitengeneza nafasi chache na hivyo hawezi kuwa na furaha licha ya kuwa matokeo si mabaya lakini wanakazi kubwa ya kufanya matapomenyana nao katika mechi ya marudiano pale Anfield.
"Tumetenngeneza nafasi chache hivyo bado tuna kazi kubwa ya kufanya jambo hili halinipi furaha" alisema Klopp
"Hata hivyo tunatakiwa kuimarika kwa sababu kuna fainali kubwa inayotukabili mbele yetu" aliongeza kocha huyo.
Liverpool inakibarua kizito cha kukabiliana na Manchester city katika mchezo wa fainali wa kombe la ligi maarufu kama "Capital One" utaopigwa siku ya jumapili ya tarehe 28 ya mwezi huu katika uwanja wa Wembley.

Comments
Post a Comment