Klopp: naitaka europa nishiriki ligi ya mabingwa Ulaya


Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema timu yake imeingia rasmi katika mbio za kushindania kombe la Europa ili waweze kupata nafasi ya kushiriki ligi ya mabingwa barani Ulaya kama ilivyokuwa kwa Sevilla.

Akizungumza na waandishi wa habari Klopp amesema kuna umuhimu mkubwa kwa timu yake kushinda taji hilo kwa sababu ana amini ndiyo nafasi pekee kwa timu ya Liverpool kupata nafasi ya kushiriki michuano ya mabingwa Ulaya.

"Timu nyingi kubwa barani zinafikiria kushinda taji hili nadhani sisi ni moja kati ya timu hizo" alisema Klopp

"Tupo katika raundi ya 32 bado mchuano  ni mgumu lakini hii ndiyo nafasi pekee ya sisi kushiriki ligi ya mabingwa Ulaya ni nafasi pekee iliyobaki"

"Timu ya Sevilla iliweza kupata nafasi hiyo na sisi tumekubali kupambana tuipate ni nafasi muhimu kwetu" aliongeza Klopp.

Liverpoo ina kibarua kizito cha kupigana na kushinda katika mechi watakaocheza leo dhidi ya FC Ausburg ya nchini Ujermani. Mashindano ya Europa yameanza kuwa na ushindi kubwa Tangu UEFA ilipotangaza rasmi kutoa nafasi kwa bingwa wa michuano kushiriki kombe la mabingwa barani Ulaya.

Comments