Kocha wa Leicester city Claudio Ranieri amewapa mapumziko ya wiki moja wachezaji wa timu yake ili waweze kurudi kivingine katika harakati za kugombania ubingwa wa ligi kuu chini Uingereza. Ranieri ana malengo ya kutwaa ubingwa baada ya kuona mwelekeo mzuri katika kikosi chake.
Ranieri ameshinda katika mpango mzima wa kutengeneza saikolojia ya wachezaji wake hilo ndilo jambo pekee ambalo limeiwezesha kuifikisha timu ya Leicester pale ilipofika, na ndiyo maana kuthibitisha hilo ameamua kuwapa likizo ndogo wachezaji wake waondokane na mawazo ya kipigo walichokipata kutoka kwa Arsenal.
Ingawa kwa sasa Tottenham Spurs wanaonekana kuwa moto ikiwa namba 2 katika msimamo wa ligi lakini wana kibarua kizito cha kuishusha Leicester pale juu, ni wazi kuna vita msimu sasa hivi kati ya Leicester, spurs na Arsenal.
Kocha wa Leicester city amefikia malengo yake katika mechi alizocheza dhidi ya Manchester city na Arsenal, Ranieri aliweka wazi kuwa alihitaji kukusanya pointi 2 pili pekee ikiwa ni kupata sare lakini akafungwa na kushinda mechi moja hivyo matokeo hayo yalizidi malengo yake baada kukusanya pointi 3.
Spurs ina kibarua cha kukabiliana na Manchester united, Arsenal, Liverpool na Chelsea wakati huu Leicester ikiwa ina kibarua dhidi ya Manchester united na Chelsea ambapo mchezo huo utapigwa katika mechi za mwisho za kufunga msimu wa ligi.
Kulingana na mtazamo wa kukamilisha ratiba nadhani Leicester city ana wakati mzuri wa kushinda mechi nyingi kuliko Tottenham, Leicester tayari imeshinda michezo dhidi ya Liverpool, Man city na tayari ameshajua hatima yake dhidi ya Arsenal nadhani ni rahis kwake kuzikabili mechi zilizobaki kuliko Spurs ambaye hajakamilisha ratiba yake dhidi ya Man united, Chelsea, Arsenal na Liverpool.
Ni wakati huu ambao naweza kusema kuwa Leicester anaweza kuwa bingwa na akaipiku Spurs yupo kwenye wakati mzuri kuliko spurs ambaye ana vibarua vine vya kukabiliana navyo. Licha ya Leicester city kuwa juu kwa pointi dhidi ya Spurs na Arsenal kama atakomaa vizuri katika mechi dhidi ya Norwich, Westbrom, Watford, Newcastle, Crystal Palace na Sunderland ana wakati mrefu wa kukusanya kabla ya kukabiliana na Manchester united na Chelsea.
Vingenevyo karata yangu nitaitupa kwa Arsenal lakini si Spurs ubingwa ukiteleza kwenye mikono ya Leicester kuna hatihati ukaangukia mikononi kwa Arsenal. kwa kutumia jicho langu la mwenye naona kuwa Leicester ana nafasi kubwa ya kuwa bingwa msimu huu.

Comments
Post a Comment