Lionel Messi ampa hat trick Suarez


Mshambulaji na nyota wa Barcelona Lionel Messi huenda akaidhihirishia dunia kuwa yeye ni  bora na wa pekee baada ya kumpa bao Luis Suarez katika ushindi wa magoli 6-1 dhidi Celta Vigo.

Bao hilo lilikamilisha idadi ya magoli matatu aliyofunga Suarez baada ya kufunga magoli mawili ya awali katika dakika ya 75 na 82 ya mchezo .

Messi alichezewa faulo katika lango la wapinzani na mwamuzi aliweka penati, alichokifanya Messi ni kupiga penati fupi akimpasia Suarez aliyekuwa nyuma yake kidogo na kufunga bao la 3 ambalo lilikamilisha idadi ya mabao 23 aliyofunga Suarez katika ligi ya La liga msimu huu.

Magoli mengine yalifungwa na Lionel Messi katika dakika ya 28, Ivan Rakitic dakika ya 85 na Neymar aliyekamilisha idadi ya goli 6 baada ya kufunga goli la mwisho katika dakika 90 ya mchezo.

Comments