Timu ya Manchester united jana ilipoteza mechi yake dhidi ya FC Midtylland baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 katika uwanja Jess Thorup nchini Denmark.
Man united ilianza kupata bao la kwanza kupitia mshambuliaji wake Mephis Depay aliyetumbukia wavuni katika dakika ya 37 lakini mchezaji wa Midtylland Pione Soste alichomoa bao hilo kabla ya kuelekea mapumziko. Kipindi cha pili wenyeji hao waliweza kupata bao la 2 kupitia Paul Onuachu na kuyafanya matokeo kuwa hivyo hadi mwisho wa mchezo..
Man united imeanza vibaya katika raundi ya 32 ya michuano ya Europa lakini bado wana nafasi kubwa ya kupita watakaporudiana nao katika uwanja wao wa nyumbani wiki ijayo. Timu zingine za Uingereza zilizokipiga jana katika michuano hiyo ni Tottenham Spurs ambayo iliambulia sare ya bao 1-1 dhidi ya fiorentina nchini Italy na Liverpool ambao hawakufungana na FC Augsburg nchini Ujermani.

Comments
Post a Comment