Timu ya Real Madrid ambayo ipo chini ya kocha Zinedine Zidane imeendelea kukumbana na misukosuko ya matokeo baada ya kujikuta ikizidi kutoa mwanya kwa Barcelona na Atletico Madrid katika mbio za ubingwa wa La liga, jana timu hiyo ikiwa katika uwanja wa nyumbani iliweza kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Atletico Madrid.
Ni wazi kuwa huenda Real Madrid ikakosa tena nafasi ya kuwa bingwa na kuziacha Barcelona na Atletico Madrid kushindania nafasi hiyo. licha ya timu hiyo kumtimua Rafael Benitez lakini hata kocha wa sasa katika timu hiyo ana wakati mgumu kama ule aiokuwa nao Benitez.
Kama Barcelona itashinda katika mchezo wa leo dhidi ya sevilla ni wazi kuwa Real Madrid itakuwa kwenye wakati mgumu kupunguzu pointi 12 ambazo Barcelona itakuwa inaongoza juu yake, wakati huu akiifukuza timu ya Atlletico Madrid kwa pointi 4 jambo ambalo ni zito kwa upande wao.
Wakati fulani niliandika ni kwanini Benitez alitimuliwa Real Madrid, licha ya watu kuwa dhana ya kuwa Perez alikuwa karibu mno na wachezaji kuliko kocha hili nililipa asilimia 40 kwa upande wangu lakini asilimia 60 zikiwa ni kushindwa kukabiliana na vigogo wa la liga.
Katika raundi ya kwanza Real Madrid haikuweza kushinda dhidi ya Sevilla, Villareal, Barcelona, Valencia na Atletico Madrid. kama unashindwa kuwatikisa tembo ambao wanaleta ushindani kwenye ligi yako basi ni wazi huwez kuwa mshindani, hili lilimtoa benitez mapema baada ya kukusanya pointi 2 pekee kwa Atletico Madrid na Valencia baada ya kupata sare katika mechi hizo huku akipoteza kwa Sevilla, Villareal na Barcelona.
Binafsi sioni matumaini ya Zidane kuwatikisa vigogo hawa katika mechi za marudiano na tayari ameanza kupoteza dhidi ya Atletico Madrid, wakati huu ana kibarua cha kupambana na Barcelona katika uwanja wa Camp Nou, Sevilla, Valencia na Villareal ni wakati ni rahis kusema Real Madrid hana dhamana ya kushinda mechi zote kwa timu waliyonayo na jinsi wanavyocheza.
Kiwango cha Barcelona kipo juu ikilinganishwa na timu zinngine za la liga, ni lini anategemewa kupoteza mechi nne mfululizo, Atletico Madrid wapo katika kiwango kizuri na wana ukuta imara wakati wote, Real Madrid anatakiwa kupambana asikose nafasi ya kushiriki ligi ya mabingwa barani Ulaya naiona ndiyo nafasi pekee iliyobaki kwao.
Leo ninaikumbuka kauli na ahadi ya kocha wa Atletico Madrid Diego Simeon ambaye alisema itakuwa ngumu kufungwa kama timu hiyo imemuuza Angel Di Maria akiamini ndiye mchezaji pakee wenye kuisumbua timu yake kama ilivyo kwa Lionel Messi Barcelona na ni wakati huu tunaona Real Madrid imekuwa na wakati wa kupata matokeo kwa Simeon.
Real Madrid inatakiwa kuandaliwa kuwa timu ili iweze kurejesha ule ufalme wake wa La liga ambao umehamia kule Barcelona, wanatakiwa kuwa na timu yenye mchanganyiko kama ilivyo kwa Benzema na Ronaldo na kwa wachezaji wote wa timu hiyo walitakiwa kuwa hivyo. jambo lisilofichika ni ngumu kwa timu ya Real Madrid kuwa mabingwa wa La liga msimu huu ni wazi wamepotea kwenye ramani ya ubingwa.

Comments
Post a Comment