Rooney amtetea LvG



Mshambuliaji wa Manchester united Wayne Rooney amesema kuwa wachezaji ndio wanaotakiwa kulaumiwa na siyo kocha wa timu hiyo kutokana na kucheza chini ya kiwango katika mchezo waliopoteza dhidi ya Sunderland.

Rooney alisema kuwa kocha wa timu huyo Louis van Gaal ana mbinu bora mazoezini lakini anashangaa wachezaji wenzake wanashindwa kuzifanyia kazi mbinu hizo badala yake wamekuwa wakicheza chini ya kiwango.

"Tulicheza chini ya kiwango katika mchezo dhidi ya Snderland na tukapoteza mchezo kwa mabao 2-1, mbinu za kocha ni nzuri mazoezini lakini tunashindwa kuzitumia ipasavyo tuwapo uwanjani"

"Hatutengenezi nafasi za kutosha na kufunga magoli, hii inatugharimu mara nyingi na siyo kosa la mwalimu, lakini mpaka mwisho malengo yetu kuhakikisha tunaingia nne bora." Aliongeza Wayne Rooney.

Manchester united imeshindwa kuwa na mwenendo mzuri  chini ya kocha huyo na kuwapo na tetesi za chini kuwa huenda nafasi ya kocha huyo ikachukuliwa na aliyekuwa kocha wa Chelsea Jose Mourinho.

Comments