soka la china linavyoteka nyota wa soka barani Ulaya.


Kama ulikua hujui nchi za Asia zimeamka na zinataka kutengeneza soka bora la vilabu katika nchi zao. China imekuwa mfano wa jambo hilo baada ya vila vyake kufanya kufuru ya usajili kwa nyota kadhaa ambao walikua wanakipiga barani Ulaya.

ligi ya China maarufu kama Chinese Super League imekuwa gumzo baada ya vilabu vyake kadhaa ikiwemo Ghoanzhou na Jiangsu Suning kufanya usajili wa kutisha katika dirisha dogo la majira ya joto. Nyota aliyekuwa anakipiga katika timu ya Chelsea Ramires tayari anayaendeleza maisha akiwa na timun ya Jiangsu Suning.

Taarifa zilizovuma siku ya jana ni kuwa kiungo maarufu wa Argentina anayekipiga katika timu ya PSG Ezequel Lavezzi amekataa ofa ya kujiunga na timu ya Chelsea na kuamua kuelekea nchini china kukipiga katika timu ya Hebei China Fortune na tayari mchezaji ameshafanya makubaliano ya awali na timu hiyo..

Ofa nono zitolewazo na klabu za timu hiyo ndizo ziwafanyavyo nyota wenye kiwango wakamalizie uko maisha yao ya soka na kuvuna utajiri. Lavezzi amewekewa mezani kiasi cha  euro 23.5 milioni akiwa na mkataba wa mshahara wa euro 400000 kwa wiki kulingana na makubaliano ya makataba atakopokuwa akikipiga katika timu ya Hebei China Fortune.

Liverpool ilitaka kumsajili kiungo mshambuliaji wa Shakthar Donetsk  Alex Texeira lakini ilishindwa kufika dau lisilopongua euro 30 milioni ili kukamilisha usajili wa mchezaji huyo ambaye alionesha nia ya kutua Anfield lakini Jiangsu Suning iliweza kufika dau la euro 38 milioni na kumsajili mchezaji uyo ambaye ameungana na Ramires katika timu hiyoo.

Akiwa amecheza miezi mitano pekee baada ya kutoka na kutua Atletico Madrid mshambuliaji Jackson Martinez alitimkia Goangzhou nchini china kwa dau la euro 32 milioni na Atletico ilishindwa kukataa dau hilo ambalo lilirudisha pesa yao.

Ramires ambaye alikuwa na wakati mgumu chini ya kocha Guus Hiddink alitimkia China January mwaka Huu kwa dau la euro 245 milioni. Wakati Asia imejipanga zaidi kuhakikisha inakua zaidi katika hata katika nchi ya India wapo nyota wengi ambao wanakipiga katika ligi hiyo na kuitangaza  ligi.

Kuna uwezekano nyota wengi zaidi wakawa wanalekea kukipia katika ligi ya nchini umo ambayo imeshilikiliwa na matajiri wakubwa wanaomwanga pesa kuitengeza na kuitangaza ligi hiyo iweze kujizolea umaarufu mkubwa duniani.

Tutegemee majina makubwa zaidi kuondoka Barani na kwenda kuvuna pesa china ili watunze zaidi akiba zao, kama Ezequel Lavezzi ambaye hajawahi hata kuwa mchezaji bora wa dunia atakuwa akipokea euro 400000 milioni kwa wiki inaweza kujenga ushawishi mkubwa kwa mastaa wa soka kukipiga katika ligi hiyo. Mpaka sasa ni Carlos Tevez pekee alinesha msimamo wa kukutaa ofa ya euro 19.5 milioni kujiunga na timu ya Shanghai SIPG.

Comments