Strika Simba na Yanga zimeweza kufunga magoli 24 kila pacha moja hadi sasa mshambuliaji wa Simba Hamis Kiiza amefunga jumla ya magoli 16 huku Ibrahim Ajib akiwa amefunga goli, katika upande wa Yanga Amis Tambwe amefunga goli 14 akifuatiwa na na Donald Ngoma ambaye ameweka nyavuni magoli 10 na kila pacha ikitimiza idadi ya mabao 24.
Simba na Yanga wanakutana jumamosi huku kila timu ikijigamba kuwa bora kuliko nyingine. Ni wakati huu ambao timu ya Simba inaonekana imefufuka baada ya kutoa vichapo vitano mfululizo katika michezo iliyomalizika.
Pamoja na pacha hizi kufunga idadi hiyo ya magoli lakini si wakati wa kutegemea mvua ya mabao katika timu hizo zitakapokutana uwanja wa taifa jumamosi ya wiki hii. Pengine Simba haitafungwa magoli 2 tena kama yale ya mchezo wa kwanza walipokutana, Pia Yanga isifungwe japo mashabiki wa Simba wana amini timu yao iko fomu na ni wakati wa kulipa kisasi.
Mnyama anategemewa kuambaza samba kutokana na kujaza viungo wengi katikati wakati huu Thabani Kamusoko na Haruna Niyonzima wanatarajiwa wanatarajiwa kufanya makubwa sehemu ya katikati.
Jackson Mayanja ambaye ni kocha wa Simba anawatumia sana Justice Majabvi, Jonas Mkude na Mwinyi Kazimoto katikati ni matumaini yangu Simba inaweza kucheza zaidi katikati kuliko pembeni, wanaweza wakautawala mpira ingawa umakini na utulivu wa Thabani Kamusoko unaweza kuliondosha hili kama watashirikiana vizuri na Haruna Niyonzima katikati.
Yanga wanaingia bila beki wao kisiki wa Kevin Yondani anayetumikia adhbu ya kukaa nje kutokana kuoneshwa kadi nyekundu katika mchezo dhidi ya Coastal ingawa Nadir Haroub atakuwemo kuna kitu kitapungua nina imani Vicent Bossou si mzoefu wa mechi hizi kama ilivyo kwa Yondani lakini kama atacheza kulingana na misingi ya soka bila shaka watakua imara kama kutakuwa na makosa kadhaa basi ni wazi Simba inaweza kupata bao la mapema la kuongoza.
Ni wakati huu ambao kocha wa Simba anawatumia Juko Mursheed na Abdi Banda kama beki wake wa kati, Hassan Isihaka amekuwa akifanya makosa mengi yalioigharimu Simba. Uwepo wake unaweza kuleta faida kubwa kwa Amis Tambwe ambaye anaweza kucheza mipira mingi ya kichwa kutokana na kimo cha Isihaka kuwa kidogo na hii inaweza kumfanya asikose Bao katika mechi hiyo. lakini kama Mayanja atamtumia Banda tambwe atakuwa kwenye mgumu wa kucheza mipira ya juu akiwa huru.
Kama Hans Pluijm atatumia 4-4-2 akiwa na Deus Kaseke, Amis Tambwe, Donald Ngoma na Simon msuva na Simba hawatarekebisha makosa yao katika safu ya ulinzi ni wazi Donald Ngoma au Amis Tambwe watacheka na nyavu.
Wachezaji wa Simba wanaona kuna faida na wanafurahi kukosekana kwa Kevin Yondani kama Simba watakuwa wanafika wengi na kushambulia kwa nguvu kiiza anaweza kuziona Nyavu, Ajibu ni fundi anahitaji beki mtulivu na makini katika kukaba, bila shaka Yanga wana imani na beki Nadir Haroub.
Mechi ni ngumu lakini nadhani washambuliaji watakaoshirikiana vizuri kucheza na udhaifu wa safu ya ulinzi ya wapinzani wao wanaweza kufanikiwa kutemresha mvua ya magoli na kuwaacha wengine wakiwa na idadi ile ya mabo 24, nadhani ni mechi ambayo haitakosa magoli labda pengine kila upande ukaongeza zaidi idadi ya magoli. Kila mmoja anataka kudhihirsha ubora wake kwenye mechi hii nadhani yapatikana mabao kwa pacha hizo za Simba na Yanga.

Comments
Post a Comment