Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limesimamisha matokeo ya ushindi wa timu ya Gold Geita SC na Polisi Tabora kutokana na kuwepo kwa kashfa ya kupanga matokeo hadi taarifa rasmi zitakopopitiwa.
Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi ya ligi ilikutana jana kupitia taarifa za mechi mbili za kundi C kati ya JKT Kanembwe na Geita Gold SC ambapo Geita Gold ilishinda ilishinda 8-0 huku katika mchezo kati ya Polisi Tabora na JKT Oljoro, Polisi Tabora iliibuka na ushindi wa goli 7-0 hali iliyopelekea utata wa kupangwa kwa matokeo.
Taarifa rasmi ni kuwa timu ya Geita Gold na Polisi Tabora zilikuwa na pointi sawa huku zikitofautiana kwa tofauti ya goli moja hali iliyopelekea kuwapo na kashfa ya kupanga matokeo kwa ajili ya kuungana na Ruvu Shooting na African Lyon ambao wamefuzu kuelekea ligi kuu.
Kulingana na katiba ya TFF Ibara ya 50(1) na (11) na Ibara ya 69 ya kanuni za TFF kanuni inabidi izingatiwe hivyo kamati ya saa 72 imemuelekeza katibu mkuu wa TFF apelike suala kwenye kamati ya nidhamu ya TFF kwa ajili ya uchunguzi ili maamuzi yafanyike.

Comments
Post a Comment