Ni jambo lisilofichika kuwa shirikisho la soka nchini Tanzania limekuwa kioja kutokana na kushindwa kufanya mambo yake kama lilivyoahidi mwanzo kabla ya kuanza kwa msimu wa ligi kuu Tanzania bara 2015/16. Ligi yetu imekuwa ikipoteza mvuto kutokana na kusimama bila mpangilio na hii imeifanya ligi yetu kuwa kama bonanza.
Lakini yote tutasahau endapo timu zetu za nyumbani zitacheza kwa ushindani na kuifanya ligi iwe yenye kupendeza. Nikiangalia mwenendo wa VPL kwa wiki mbili zilizopita inatia hamasa kutokana na ushindani uliopo, naingalia Coastal, Ndanda, Prisons, Simba na mtibwa na hata Stand united zinapambana kuleta ushindani wa hali juu.
Tofauti na msimu ulipoita kufikia raundi hii 2 imekuwa ya tofauti ni vigumu kutabili nani atakuwa bingwa, Yanga imepoteza pointi 5 dhidi ya Coastal na Prisons, Simba imerudi fomu na kukusanya idadi ya pointi 42 ikiwa imezidiwa pointi moja na Yanga yenye pointi 43, Azam inalingana na Simba lakini bado ina michezo 2 mkononi.
Naiona nafasi ya ubingwa kwa mtibwa pia, ligi imekuwa ya ushindani kama ilie ligi maarufu ile EPL ambapo leo Leicester yuko juu akiwaumiza vichwa vigogo wa Uingereza. Nimehamasika kuiagalia VPL kwa nguvu zote kwa sababu inaniondolea kichefuchefu cha kujua nani bingwa kama ilivyo kule Bundesliga ambapo Bayern Munich imekuwa ikitangaza ubingwa mapema.
Imetutoa kule kwa kina Zlatan Ibrahimovich ambapo PSG anaongoza kwa pointi 30 hadi sasa, ambapo Mshambuliaji Ibrahimovich anaongoza kwa magoli 23 anayemfuata akiwa na goli 12.
Angalia hapa nyumbani Amis Tambwe anaongoza kwa goli 13 pamoja na mshambuliaji wa Simba Hamis Kiiza, akifuatiwa na Donald Ngoma pamoja Jeremia Juma wa Coastal union mwenye goli 9 bila kumsahau Elias Maguli. Kwa ushindani huu tunasahau vile vioja na vichekesho vya TFF.
Pamoja na mapungufu yatokanayo na mwongozo wa ligi yetu lakini timu zetu zinatakiwa kujitoa na kucheza kwa ushindani ili kuleta mvuto wa ligi kwa mashabiki wetu wa Tanzania, nadhani huu ni wakati wa timu zinatakiwa kuonesha ubora wao ili tusahau vioja vya pale Karume.

Comments
Post a Comment