Ukizungumzia mchezji na kiungo bora katika ligi ya Vodacom bila shaka huwezi kumwacha Thabani Kamusoko ambaye amenyakua tuzo ya mchezaji bora wa mwezi. uwepo wa Thabani Kamusoko unaifanya yanga kuwa na soka la uhakika na la kueleweka wakati wote.
Yanga imeshindwa kutamba vizuri katika sehemu ya katikati katika mechi 3 za mwisho ilizocheza bila Thabani Kamusoko, hapa namaanisha dhidi ya Coastal Union, Prisons na JKT Ruvu. katika michezo hii Juma Said alishindwa kuunda safu bora ya kiungo na Haruna Niyonzima na hiyo iliwapelekea Yanga kupoteza mechi 2-0 dhidi ya Coastal ambapo Coastal ilitawala mchezo katika vipindi vyote vya mchezo.
Kamusoko ambaye anacheza namba 6 na 8 kulingana na kocha Pluijm atakavyopanga ni fundi wa kutulia na mpira katikati, kuchungulia mashimo na uwepo wake huifanya timu yanga kuutawala mpira katika muda mwingi wa mchezo.
Kukosekana kwa Thabani Kamusoko kumeonesha ni wazi kamusoko ni muhimili katika safu ya kiungo ili Yanga iweze kufanya vema zaid. Naikumbuka ile sare dhidi ya Prison kule mbaya Niyonzima alimwitaji sana Kamusoka kuliko Terera na Juma Said ili Yanga ijihakikishie ushindi dhidi ya Prisons ambao huwa wagumu wa kupoteza matokeo katika uwanja wao wa nyumbani.
Licha ya ushindi wa mabao 4-0 ambao Yanga ilipata shida katika eneo la katikati dhidi ya JKT Ruvu, baada ya Ruvu kuonesha soka maridadi katika safu ya kiungo kulingo yanga ambao walicheza zaidi pembeni, Hii inadhihirisha wazi kuwa kiungo Thaban Kamusoko kutoka nchini Zimbabwe ni shida akiwapo eneo la katikati kuliko uwepo wa Salum Terera au Juma Said kama mmoja kati yao atacheza na Haruna Niyonzima.

Comments
Post a Comment