Baada mshambuliaji wa Tanzania Adi Yusuph anayekipiga katika timu ya Mansfield nchini Uingereza kujiunga na taifa stars nyota Mwingine aliyekuwa akikipiga nchini humo amerejea kuongeza nguvu stars.
Abbas Pira 28, ambaye alicheza timu ya Coastal Union 2002/2003 ni mzaliwa wa Tanga eneo la barabara 3 amecheza katika ya Hillington FC, Wibledon na Kiliburn FC tangu atue Uingereza mwaka 2006 kwa ajili ya Elimu ya juu akiwa na umri wa miaka 17.
Mafanikio ya nahodha wa timu ya taifa Mbwana Samatta yamekuwa chachu na kivutio kwa nyota wengine wanaocheza nje ya Tanzania kuanza kujitokeza kama wafanyavyo wachezaji wa nchi zingine wanaocheza nje ya nchi zao.
Abbas Pira ni mtoto wa tajiri Gulam Pira anayemiliki visima vya mafuta jijini Tanga. Licha ya kuchezea timu hizo akiwa Uingereza pia mchezaji huyo amewahi kufanya majaribio katika timu ya Chelsea, MK Dons na Birmingham city lakini kwa kuwa Tanzania haikuwa na vigezo kutoka na kuwepo chini ya zile nafasi 70 katika viwangi vya soka duniani.
Mchezaji huyo amerejea nyumbani rasmi kuendelea na maisha yake soka hapa nchini na anatamani kupata timu ya kuchezea katika moja ya timu za ligi msimu ujao.

Comments
Post a Comment