Vijana 450 wafanyiwa majaribio Azam


Timu ya Azam imeanza zoezi la lake la kusaka vipaji mtaani jana kwa mara ya kwanza iliwajaribu vijana 450 ambao walifika Chamanzi Complex.

Azam kupitia msemaji wake Jaffar Iddi kama alivyosema wiki iliyopita timu  hiyo ilianza kufanya mchujo kwa Vijana wa wilaya ya Kigamboni na Temeke ambao jana walifika Chamanzi.

Pia zoezi litahamia Ilala ambapo vijana katika wilaya hiyo watafanyiwa majaribio Septemba 3 mwaka huu katika uwanja wa JMK na mwisho watamalizia na Wilaya ya Kinondoni katika viwanja vya Kawe.

Mbali na Dar es Salaam Azam itahamia katika mikoa ya Mwanza, Kigoma, Arusha, Tanga na Zanzibar wakiendelea na zoezi hilo la kusaka vipaji.

Timu hiyo imewahi kuibua vipaji mbalimbali kupitia timu yao ya Vijana akiwemo Faridi Mussa na Himid Mao ambao wanafanya vizuri kwenye uwanja wa soka duniani.


Comments