Timu ya Yanga imejichimbia katika hoteli moja maarufu ikijita rasmi kambini ili kujiandaa na mtiririko wa mechi zinazowakabili kwa muda wa siku kumi.
Mfululizo wa mechi hizo ambazo zinawakabili Yanga ni kutokana na malimbikizi ya viporo vya mechi tatu ambazo Yanga ilishindwa kucheza kutokana na mpangilio mbovu wa ratiba ya TFF, hatua ambayo iligomewa na Simba ikiita TFF ikamilishe viporo vya Yanga na Azam hadi watakapokuwa sawa ndipo watakaposhiriki kuendelea na mechi za ligi.
Shikizo la muheshiwa waziri wa habari, utamuduni na michezo Nnape Nnauye ndiyo lilipolekea presha kwa TFF ambao wametakiwa kuhakikisha Yanga na Azam inakamilisha ratiba zao ili kuwepo kwa usawa baina ya timu hizo.

Comments
Post a Comment