Mshambuliaji wa Tottenhma hotspurs Harry Kane ameweka rekodi katika timu yake baada ya kutupia nyavuni bao la kusawazisha dhidi ya Liverpool katika uwanja wa Anfield.
Kane ambaye jana alikuwa amefunga bao la 22 amekuwa mchezaji wa kwanza kufikisha idadi hiyo magoli kwa msimu baada ya kuwapiku Gareth Bale na Teddy Sheringham ambayo ndiyo walikuwa wamefunga magoli mengi kwa msimu mmoja ambapo wote kwa pamoja walifunga idadi ya magoli 22.
Kane amekuwa Gumzo kwa ufungaji tangu alipoibuliwa rasmi na Sharewood hadi leo chini ya kocha Mauricio Pochettino jambo ambalo ambalo limekuwa likizitoa udenda timu kubwa duniani kama Manchester united na Real Madrid.
Kwa idadi hiyo ya magoli inamfanya Kane kuongaza kinara cha wafungaji akiwapiga chini Riyad Mahrez, Jamie Vardy na Sergio Aguero.

Comments
Post a Comment