Timu ya Leicester city imekata mzizi wa fitina baada ya kusimama kwa pointi juu ya msimamo wa ligi kuu Uingereza baada ya kuichapa Southampton kipigo cha bao 1-0.
Leicester ambayo hadi jana ilikuwa imekusanya pointi 69 ipo katika nafasi nzuri ya kupigania ubingwa baada ya kuicha Tottenham kwa pointi 7 kutokana na matokeo ya sare waliyoyapata dhidi ya liverpool.
Kocha wa timu hiyo Claudio Ranieri amesifu jitihada za pekee zinazofanywa na wachezaji wake ambao wamekuwa wakijituma wanapokuwa na hiyo ndiyo nguzo pekee inayowafanya wafikie malengo yao ya kupigania ubingwa wa EPL.
"Watu wengi walikua wakisubiri nini kitatokea kwetu baada ya Tottenham kutoa sare na liverpool lakini nadhani sasa wameshapata majibu tupo kwenye nafasi gani." Alisema Ranieri
Bao pekee la Leicester lilifungwa na beki na nahodha wa timu hiyo Wes Morgan dakika ya 38 lilitosha kuipa timu pointi 3 na kujihakikishia nafasi nzuri ya kuendelea na mbio zao za ubingwa.

Comments
Post a Comment