Kiungo wa timu ya Leicester city ya Uingereza Riyad Mahrez amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka katika ligi ya EPL ambapo jana aliitwaa tuzo hiyo (PFA).
Mahre ambaye amefunga magoli 17 hadi kufikia jana amekuwa msaada kwa Leicester kufanya vizuri katika ligi Msimu huu na kuifanya Leicester city kuwa katika nafasi nzuri ya kupigania ubingwa wa ligi kuu Uingereza hadi sasa.
Mahrez ameungana na mchezaji wa Tottenham hotspurs Delle Alli ambaye amebeba tuzo hiyo kwa upande wa wachezaji wanaochipukia Uingereza na kuwazidi kete Phelipe Coutinho wa Liverpool pamoja na mchezaji mwenzake Harry Kane.
Tuzo hiyo inaweza kuongeza chachu kwa Barcelona na timu zingine kumwania mchezaji huyo ambaye amekuwa kwenye ubora katika kipindi chote msimu huu tangu atue Uingereza.

Comments
Post a Comment