Kwa lugha rahis ni kwamba Ufaransa imefufuka sasa kutokana na kuwapo kwa kizazi cha watu wa mpira. Tangu 2006 Ufaransa ilimomonyoka na haikuweza kuwa kufanya vizuri kwenye mashindano kutokana na kupotea kwa wachezaji bora wa mpira miguu.
Lakini wakati huu ambao Ufaransa imetimia kuanzia nyuma hadi mbele nikimaanisha safu zote tatu yaani ulinzi, kiungo na Ushambuliaji. kwa mafano karimu Benzema ni chaguo la kwanza la kocha wa Ufaransa lakini chaguo la pili ni Oliver Giroud ikumbukwe kuna Alexandre Lacazzate wa Olymic Lyon pamoja na C'edric Bakambu ambaye amekuwa kwenye wakati mzuri na Villareal.
Natamani kuingolea Ufaransa kwa Ujumla lakini napenda nizungumzie sehemu ya Kiungo napenda kumzungumzaia kiungo nayefanya vizuri Uingereza kwa sasa Ngo'lo Kante anyekipiga katika timu ya Leicester City, bila shaka wanao fahamu kazi yake ni wazi kijana huyu habahatishi.
Kama Claudio Ranieri angempoteza Ngo'lo Kante kwa miezi miwili kwa majeraha au sababu zingine basi ni wazi ingekuwa ngumu kuwepo kwenye nafasi ya kuwania kwa sasa. Namkubali pia Muingereza Drink Water lakini bila mafaransa huyu asingeweza kuwa kwenye wakati mzuri na timu ya Leicester.
kocha wa Ufaransa amezungukwa na watu wa mpira katikati lakini mpaka sasa simnyimi nafasi staa wa Juventus Paul Pogba ambaye amekuwa muhimili kwenye timu hiyo, lakini kuna Blaise Matuidi, Dimitri Payet, Antoine Griezman, frank Ribery, Morgan Scheiderlin, Moussa Sissoko, Yohan Cabaye, Geofrey Kondogbia, Lassana Diara na wengine wengi ambao wanampa mwalimu kibarua.
N'golo Kante 25 ana uwezo mkubwa kukaba, amekuwa amekuwa akikaba bila kufanya makosa ya kuigharimu timu yake na anaweza kusaidia mashambulizi katika ngome pinzani na ana pasi zilizo bora uwanjani. Nadhani mwalimu anaweza kuamua kumpa nafasi Kante mbele Geofrey Kondogbia na Morgan Scheiderlin.
Kama Kante atacheza na Pogba katika sehemu ya kiungo nadhani Ufaransa itakuwa bora zaidi, wote wana kasi na kasi yao inaendana, mimi binafsi sioni nafasi ya N'golo Kante kusubiri katika benchi. Leo kante anafanya kazi tatu pale Leicester kwanza anakaba, pili ana uwezo wa kuiongoza timu kwenye mashambulizi na kupiga pasi wakati huu Pogba anauwezo wa kukaba na kuendesha timu nadhani ni kabarua cha mwalimu Ufaransa kumtafuta kiungo atakaeichezesha timu hiyo.
Ingawa sijui Didier Deschamps anafikilia nini kwenye kichwa chake lakini siamini kuachwa kwa N'golo Kante lakini siamini kama atakosa nafasi katika timu hiyo nina imani anaweza kufanya kazi ambayo haiwezi kufanya na Morgan Scheisderlin, Yohan Cabaye na Blaise Matuidi huenda akawa na kibarua dhidi ya Geofrey Kondogbia anayekipiga katika timu ya Intermilan..

Comments
Post a Comment