Puma kuingia mkataba na faridi


Kiungo wa timu ya Azam Farid Mussa amepokea mkataba wa awali wa kampuni ya vifaa vya michezo ya nchini Ujermani maarufu kama Puma.

Ingawa mkataba huo siyo rasmi mchezaji huyo ameanza kupokea vifaa vya awali ikiwemo viatu pea nne na track suit na yuko mbioni kuelekea nchini Hispania kwa ajili ya kufanya matangazo na kumalizana rasmi masuala ya mkataba na kampuni hiyo.

"Ni kweli nimepokea mkataba rasmi na kampuni hiyo na tayari wameshatuma vifaa vya ikiwemo viatu pea nne vyenye thamani ya shilingi milioni moja na nusu pamoja na track suit ambazo huwa navaa nje ya mazoezi." Alisema.

"Mkataba huu siyo rasmi lakini upo mpango wa maandalizi ya safari kuelekea nchini Hispania ili nimalizane na kampuni hiyo." Aliongeza Faridi.

Kampuni ya puma iliyoanzishwa mwaka 1924 imekuwa ikidhamini vifaa vya michezo kwa wachezaji mbalimbali duniani wakiwemo baadhi ya nyota maarufu duniani kama Sergio Aguerowa Manchester city na Oliver Giroud wa Arsenal.


Comments