Samatta atupia, Genk ikiua 2-1.


Raia wa Tanzania anayekipiga katika timu ya Genk Mbwana Samatta jana aliweza kufunga bao lingine na kuifanya Genk kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Samatta alitupia goli katika dakika ya 8 ya mchezo likiwa ni goli lake la nne tangu alipojiunga na miamba hiyo Ubelgiji tangu asajiliwe akitokea timu ya TP Mazembe.

Samatta ambaye amewahi kuwa mfungaji bora katika ligi ya mabingwa Afrika amekuwa na wakati mzuri tangu ajiunge timu hiyo na jana aliweza kucheza kwa dakika zote 90.

Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Tanzania ameanza kuwa balozi wa kuitanga nchi yetu, huenda kukawa na nafasi zaidi kwa wachezaji wengine wa Tanzania kufuatiliwa na timu za Ubelgiji.

Comments