Yanga yaelekea Pemba kuiwekea Al-Ahly kambi


Baada ya ushindi wa goli 3-1 dhidi ya Kagera Sugar timu ya Yanga imepanda boti kuelekea visiwani Pemba kuweka kambi ili kujindaa na mechi dhidi ya Al-Ahly.

Yanga itashuka dimbani jumamosi ya wiki kuikabili Al-ahly katika uwanja wa taifa ikiwa na kibarua cha kukabiliana na timu hiyo katika mchezo wa marudiano utakaopigwa April 19 mwaka huu,

Mwaka 2014 timu hizo zilikutana katika hatua ya mtoano ambapo Al-Ahly iliwatoa Yanga kwa mikwaju ya penati katika mchezo wa marudiano uliopigwa nchini Misri.

Timu ya Yanga imeungana na mchezaji wake Nadir Haroub ambaye anaonekana kuwa fiti baada kuwa nje akiuguza majeraha yake na sasa amerejea rasmi kikosini.

Comments