Timu ya Arsenal inajiandaa kuweka mezani kitita kisichopungua euro 30 milioni ili kuinasa saini ya mshambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge.
Arsenal imefikia uamuzi huo kutokana na kukosa mshambuliaji mwenye makali msimu huu hali iliyopelekea timu hiyo kukosa ubingwa.
Oliver Giroud na Theo walcott ambao walipewa dhamana ya kubeba jukumu la kufunga msimu huu bado wameshindwa kuwa makali na msimu kama ilivyo kwa Harry Kane wa Tottenham Hotspurs na Jamie Vardy wa Leicester city.
Mbali na Sturridge kukumbwa na majeraha ya mara kwa mara msimu huu lakini ana kipaji cha kufunga aingiapo uwanjani jambo linalomvutia Arsene Wenger aweze kufanya usajili wa mchezaji huyo.

Comments
Post a Comment