Arsenal yakamilisha usajili Xhaka


Timu ya Arsenal leo imekamilisha dili la kumsajili kiungo wa timu ya Borrusia Moncheglabach Granit Xhaka.

Xhaka atajiunga rasmi na timu ya Arsenal Juni 1 mwaka baada ya kufunguliwa rasmi kwa dirisha kubwa la usajiri.

Arsenal wamelipa dau lisilopungua euro 30 milioni na kufanikisha dili la Mswisi huyo ambaye ataungana na timu yake ya taifa katika michuano ya UEFA Euro itakayoanza Juni 10, mwaka huu.

Xhaka 23, alipanda ndege ijumaa iliyopita kuelekea London kufanya makubaliano binafsi na timu hiyo kabla ya kuungana na wachezaji wenzake kwenye timu ya Taifa.


Comments