Timu ya Barcelona imeonesha kuwa haishikiki nchini Hispania baada ya kuichapa jana Sevilla mabao 2-0 katika fainali ya kombe la mfalme.
Barcelona ilienda sare na Sevilla hadi dakika tisini ambapo katika muda wa nyongeza timu hiyo ilipata magoli kupitia Jordi Alba aliyefunga dakika ya 97 na Neymar katika dakika ya 120.
Barcelona ilionekana kujipanga vyema kwenye safu ya ulinzi licha ya Javier Mascherano kupewa kadi nyekundu katika dakika ya 32 kipindi cha kwanza kabla ya kiungo wa Sevilla Ever Banega kupokea kadi nyekundu kwenye dakika ya 90.
Kwa taji hilo la jana sasa Barcelona imekusanya jumla ya mataji 90 tangu ianzishwe na kuitupa Real Madrid yenye mataji 82 katika michuano ya ligi na mataji mbalimbali barani Ulaya.

Comments
Post a Comment