Mshambuliaji wa Christian Benteke huenda akaondoka Liverpool baada ya kukosa namba ya kudumu tangu asajiliwe na timu hiyo.
Benteke ambaye alisajiliwa na Brendan Rodgers akitokea Aston Villa ameshindwa kuwika tangu ajiunge na majogoo hayo ya Anfield jambo pekee linalofungua milango kwa timu zingine kumsajili.
Benteke 25, ameshindwa kufiti katika mfumo wa kocha Jurgen Klopp ambao unatumia kasi kubwa uwanjani dhidi ya Mbelgiji mwenzake Divock Origi na Daniel Sturridge ambao wamekuwa chaguo namba moja la Klopp.
Kurudi kwa mshambuliaji wa Liverpool Danny Ings ambaye alikuwa majeruhi kwa muda mrefu kunafuta matumaini ya Benteke kutamba katika timu ya Liverpool Huenda mshambualiaji huyo akaondoka na Tayari timu ya Juventus imeanza kumtolea macho.

Comments
Post a Comment