Brendan Rodgers apata kibarua Celtic


Aliyekuwa kocha wa zamani wa timu ya Liverpool  Brendan Rodgers sasa atakuwa akiionia Celtic ya Scotland baada ya kusaini mkataba.

Rodgers 43, amesaini mkataba wa miezi 12 kuinoa timu hiyo, akiwa anakaribia kumaliza mwaka mmoja tangu Liverpool iachane nae.

Rodgers ambaye alikuwa na msimu mzuri na Liverpool 2013/14 ana amini zaidi katika vijana, huenda akainua zaidi vipaji katika timu hiyo kama ilivyokuwa kwa Raheem Sterling pale Liverpool.

Comments