Licha ya kubembelezwa na raisi wa TFF Jamal Malinzi nahodha wa zamani wa timu ya taifa Nadir Haroub 'Cannavaro' amekataa kurejea tena kwenye timu ya taifa.
Baada ya kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa ndani barani Afrika kocha wa taifa Stars Bonifasi Mkwasa alimtangaza rasmi Mbwana Samatta kuwa nahodha mpya wa timu ya taifa.
Uamuzi huo ulimfanya mlinzi huyo wa timu ya Yanga aliyekuwa majeruhi wakati huo kuustafu rasmi kuichezea timu ya taifa.
Timu ya Taifa iko mbioni kuelekea Nairobi kuchuana na timu ya taifa ya Kenya 'Harambee Stars' katika mchezo wa kujipima nguvu kwa ajili ya kujiandaa na mechi ya kufuzu michuano ya CAN dhidi ya Misri.

Comments
Post a Comment