Kocha wa England Roy Hodgson amebaki na kikosi chake kamili atakachokwenda nacho Ufaransa baada ya kuwatema wachezaji watatu.
Baada ya mechi tatu za mchujo Hodgson amewatema rasmi Fabian Delph, Andros Townsend na Danny Drinkwater baada ya kutangaza orodha ya wachezaji 23 mapema leo hii.
Damian Delph ameondolewa kutokana na kuumia mazoezini hata hivyo kocha wa England hakuridhishwa na kiwango kilichooneshwa na Danny Drinkwater na hivyo aliamua kumwondoa rasmi mchezaji aliyekuwa kwenye wakati mzuri na timu ya Leicester.
Licha ya Daniel Sturridge kuhusika kwenye hofu ya kuingia kwenye majeraha lakini mchezaji huyo amehusihwa kikosini baada ya kurejea mazoezini jana na sasa ataungana na mshambuliaji kinda wa Manchester united Marcus Rashford, Wayne Rooney, Harry Kane pamoja na Jamie Vardy.

Comments
Post a Comment